• Conference Venue-Sea Cliff Hotel & Spa
  • Meli hii ni sehemu ya kukutania pia
  • Conference Venue Sea Cliff Hotel & Spa

Maandalizi Ya Kongamano La Diaspora Yapamba Moto Zanzibar..

Image may contain: 2 people, people sitting and indoor

Pichani kulia, Mheshimiwa Issa Haji Ussi Gavu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akiongoza kikao cha Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la Diaspora jana Kisiwani Zanzibar. Kongamano hilo la siku mbili litafanyika wiki hii, Jumatano na Alhamisi ( Agosti 23-24) kwenye Hotel ya Sea Cliff And Spa. Kulia kwa Mheshimiwa Gavu ni Mheshimiwa Hassan Hafidh, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka jimbo la Welezo na ni mdau wa Diaspora.
Wahi fursa hii kwa kujiandikisha kuhudhuria online..http://tzdiaspora.org/registration.html

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajia kufanya Kongamano la nne la kitaifa la Watanzania wanaoishi Ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) kuanzia tarehe 23 hadi 24, hapa Zanzibar.

Kongamano hilo ni mwendelezo wa makongamano matatu ya awali yaliyofanyika mwaka 2014 na 2015 huko Dar es Salam na 2016 lililofanyika hapa Zanzibar.

Lengo kuu la makongamano hayo ni kwa Serikali na wanadiaspora kukutana, kubadilishana mawazo na kuwashajihisha wanadiaspora kuwekeza nchini kwao kwa maslahi yao na kwa ustawi wa uchumi wa taifa lao.

Kongamano hilo linatarajiwa kuwashirikisha washiriki wapatao 350, ambapo miongoni mwao wanadiaspora wanakadiriwa kuwa 200 na watendaji kutoka taasisi za Serikali zote mbili wanatarajiwa kuwa 150.

Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa kongamano hilo ambao unatarajiwa kufanyika katika hoteli ya Sea Clif Resort and Spa liyopo katika kijiji cha Kama Wilaya ya Magharibi A.

Kongamano hili la nne litabebwa na dhamira ya “Uzalendo kwa Maendeleo” chini ya kauli mbiu isemayo “Mtu Kwao, Ndio Ngao

 Click here to Register

Our Sponsers

contact us

Dar es Salaam, Tanzania

Call Us: +255784270403

Visitors Counter

244749
Today
This Week
This Month
All days
59
446
3905
244749