• Conference Venue-Sea Cliff Hotel & Spa
  • Meli hii ni sehemu ya kukutania pia
  • Conference Venue Sea Cliff Hotel & Spa

BALOZI PHILIP SANKA MARMO AAGWA NA BABA MTAKATIFU PAPA FRANCIS BAADA YA KUMALIZA MUDA WAKE

ARO

Aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Philip Marmo ameagwa rasmi jana na viongozi wa Vatican, balozi huyo aliyekuwa na makazi yake jijini Berlin, alikuwa anahudumu nchi 10 na nafasi yake hivi sasa itashikiliwa na balozi Abdalah Possi ambaye aliapishwa jana na Rais Dk John Magufuli.

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani aliyemaliza muda wake, mheshimiwa Philip Sanka Marmo ambaye alikuwa anahudumia nchi 10 ikiwemo Vatican, akiagana na Baba Mtakatifu Papa Francis jana baada ya kustaafu utumishi wake, (kulia) ni mke wake mama Nuruana Marmo.

ARO 1

Baba Mtakatifu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis akimpa zawadi mama Nuruana Marmo, mke wa Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, balozi Philip Marmo aliyemaliza muda wake ambaye alikuwa anahudumia nchi 10 ikiwemo Vatican, mama Nuruana Marmo, wakati walipofika jana kwa ajili ya kumuaga Papa.

ARO 3

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani aliyemaliza muda wake Philip Marmo akiagana jana na Mkuu wa Utawala, Vatican (Secretary of State), Mhadhama Kardinali Pietro Parolin, balozi Marmo alikuwa anatumikia nchi 10 ikiwemo Vatican.
ARO

Balozi Philip Marmo akiagana na Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano na Mataifa (Secretary for Foreign Relations with States), Askofu Mkuu Paul Callagher, alipofika jana kuagana na viongozi wa Vatican, balozi Marmo ambaye alikuwa na makazi yake jijini Berlin nchini Ujerumani alikuwa anahudumia nchi 10 ikiwemo Vatican.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajia kufanya Kongamano la nne la kitaifa la Watanzania wanaoishi Ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) kuanzia tarehe 23 hadi 24, hapa Zanzibar.

Kongamano hilo ni mwendelezo wa makongamano matatu ya awali yaliyofanyika mwaka 2014 na 2015 huko Dar es Salam na 2016 lililofanyika hapa Zanzibar.

Lengo kuu la makongamano hayo ni kwa Serikali na wanadiaspora kukutana, kubadilishana mawazo na kuwashajihisha wanadiaspora kuwekeza nchini kwao kwa maslahi yao na kwa ustawi wa uchumi wa taifa lao.

Kongamano hilo linatarajiwa kuwashirikisha washiriki wapatao 350, ambapo miongoni mwao wanadiaspora wanakadiriwa kuwa 200 na watendaji kutoka taasisi za Serikali zote mbili wanatarajiwa kuwa 150.

Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa kongamano hilo ambao unatarajiwa kufanyika katika hoteli ya Sea Clif Resort and Spa liyopo katika kijiji cha Kama Wilaya ya Magharibi A.

Kongamano hili la nne litabebwa na dhamira ya “Uzalendo kwa Maendeleo” chini ya kauli mbiu isemayo “Mtu Kwao, Ndio Ngao

 Click here to Register

Our Sponsers

contact us

Dar es Salaam, Tanzania

Call Us: +255784270403

Visitors Counter

256447
Today
This Week
This Month
All days
20
1711
7123
256447